Kwi kwi kwenye libeneke la blogu ya Issa Michuzi linatatuliwa
16 years ago | 3058 reads
nachukua nafasi hii kutoa asante kwa mh. kunitembelea na wakati huo huo kutoa ufafanuzi na kuomba radhi wadau wote kwa kwikwi iliyotuandama juma zima.
ni kwamba, katika juhudi za kufanya globu ya jamii iwe bora zaidi, tumepata server ambayo ina nafasi kubwa hata za kuanzisha libeneke la video kama tulivyoahidi awali. tatizo linakuja kwamba mitambo ya host wetu inakuwa ikiteleza mara kwa mara kudaka link ya globu ya jamii na kusababisha kwikwi ya mara kwa mara.
na ili kukomesha kwikwi hiyo imeonekana bora tuendeleze libeneke kwenye anuani ya issamichuzi.blogspot.com kama ilivyokuwa zamani wakati tukisubiri wahandisi wa host wetu arekebishe mambo.
kunradhi kwa usumbufu unaowapata wadau na nashukuru kwa jinsi maelfu ya wadau wanavyolifuatilia swala hili na kunipa moyo kuwa nisikate tamaa. nami naahidi kuendeleza libeneke bila kusita pamoja na kukumbwa na changamoto za kiufundi ambazo ziko nje ya uwezo wetu.
natumai mtaendelea kutuelewa na kutuvumilia
Source: issamichuzi.blogspot.com