Nimeshangaa hata kutoamini macho yangu kipindi tupo twasikiliza redio kutangazwa baraza la Mawaziri , Dkt John Pombe Magufuli alikuwa hapa kwenye Ujenzi wa daraja la Kigamboni na tena akiwa peke yake kavaa casual alikuwa ana-drive Gari lake mwenyewe. Watu wamecheka na kufurahi kwa vile kaondoka pale kwenda kukagua eneo lenye utata wa kupisha Ujenzi. inaonekana  alikuewa hata hajui kinachoendelea Ikulu!
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Muheshimiwa J.P. Magufuli anapiga kazi! Hao ndiyo aina ya watendaji ambao lazima JK ajivunie sana katika serikali yake....Magufuli ni aina ya kiongozi ambaye hata dhamiri za watu wa kawaida kabisa mtaani wanamkubali...anaweza akawa na weaknessses kama binadamu mwingine yeyote (maana hatutarajii kama atakuwa perfect kama malaika, yeye ni binadamu) lakini ki-ukweli na bila kutafuna maneno Hon. J.P. Magufuli yuko vizuri, ni mchapa kazi!

    ReplyDelete
  2. Tunahitaji watu wanaotimiza wajibu wao kama Dr. Magufuli. Wakati wengine wakingojea kupewa vyeo wakistarehe na kusikiliza na kuangalia TV, mwenzao mchapa kazi alikuwa kazini akitimiza wajibu wake. TUNAHITAJI MAWAZIRI WATANO KAMA MAGUFULI AKIWAMO WAZIRI MKUU MPYA ili nchi iweze kupiga hatua. Mawaziri wengi waliopo na waliochaguliwa wanajali matumbo yao. NANI KAMA MAGUFULI?

    ReplyDelete
  3. Mjomba Michuzi tarehe umeiona ktk hii habari?

    Leo ni Jumatatu tarehe 20 Januari, 2014 wewe umeweka Jumatano tarehe 29 Januari ,2014 !!!

    ReplyDelete
  4. ingekuwa si siasa yetu huyu angefaa kumrithi jakaya lkn wenye siasa chafu watampiga vita najua lkn magufuli jembe hataki mchezo ktk kazi

    ReplyDelete
  5. Mhe. Dr. John Pombe Magufuli CHAPA YA CHUMA kiboko yao hana wasiwasi na matokeo yeyote kufuatia Upanguaji wa Baraza la Mawaziri kwa vile anajua anachokifanya sio cha kubabaisham, anafanya kazi inavyo stahili atakaye mchukia atakuwa ni Fisadi.

    Hivyo anajua Mchapa kazim mwezake Jakaya Kikwete hawezikumweka kando!

    ReplyDelete
  6. The mdud,unajua mie nashidwa kuelewa why CCM wasimsimamishe huyu waziri na wakashinda kwa kishindo na hata kwenye kampeni wala wasingesumbuka sn,,cha ajabu mijitu isio chapa kazi na kua na uchungu wa nchi yao ndio eti wa kwanza kuanza kampeni za urais lo washindwe wao na walegee na wawe na uzito wa pamba au sufi,watanzania wenzangu tuamkeni na tuwapime hao watu wapi wametoka,wapi walipo,na wanaelekea wapi? Labda nikupeni watu ambao wako tayali kuiokoa nchi yetu tena nawataja pasipo na kificho,,Rais Magufuli,w,mkuu Rowasa,waziri wa uchumi na pesa Ripumba naibu wake John mashaka,waziri wa nishati na madini Zitto,Mwakiyembe Elimu na ufundi maana elimu ya sasa ni kituko ila akiwa huyo mambo juu ya mambo,usalama wa taifa dr slaa,mambo ya ndani Sefue,wa nje abaki yeye,utalii na mapambo ya mijini ni S Sitta,Mama Kilango na Mwigilu wapewe ustawi wa jamii na watoto,ndugu zanguni nilipo kosea mtanilekebisha na waliobaki mtanisaidia,,KARIBUNI TULIJADILI HILI SWALA,nimeyasema hayo yote nikiwa na machungu yasio isha,KWA NINI KILA MWAKA TUNAZIDI KUDONDOKA KIUCHUMI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...