Hili lilikuwa igizo lililoendeshwa na askari polisi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman mjini Unguja jana Jumapili Januari 12, 2014.


"Askari wa kikoloni", akipewa adhabu ya push up baada ya kuboronga wakati wa gwaride. Hili lilikuwa igizo lililoendeshwa na askari polisi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa michezo Aman mjini Unguja Jumapili Januari 12, 2014.

Kamanda wa kikosi cha askari KAR, akiongoza wenzake kwenye onyesho la Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi lililoendeshwa na askari polisi kuonyesha jinsi jeshi la kikoloni lilivyokuwa likifanya mambo yake,enzi hizo na ilikuwa ni burudani nzuri sana iliyomvutia kila aliekuwa akitazama.
Kwa picha zaidi ya siku hii BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kweli mkoloni hakuwa na 'Mswalie Mtume' Ama kweli oppression inapozidi ku-resist ni lazima na sio option. Udumu Muungano, MAPINDUZI DAIMA!

    ReplyDelete
  2. Tunaomba Video Clip ya hiki kikosi cha Jeshi ili na sisi wa mbali tuweze kuwaona, Plz ...Plz

    ReplyDelete
  3. Tuwekee ka clip bas tufaidi vizuri ankal jamani

    ReplyDelete
  4. Kweli askari wa 'KEYA' na kofia zao za 'KEYA' a.k.a KRA King's AFRICAN RIFLE physique yao namba moja ilikuwa kutisha Jamii. Hakika hili ni somo zuri la kihistoria.

    Si bure sasa tuna Jeshi La Wananchi ambalo ni jeshi la kulinda Wananchi na mipaka ya Jamhuri ya Muungano.

    Mdau
    Mkongwe

    ReplyDelete
  5. Ohooo Askari wa KAR ilikuwa si mchezo!

    Babu yangu alinieleza ya kuwa wakati wa Kukusanya Kodi walipokuwa vijana walikuwa wakiwaona Askari wa KAR wanakuja watu walikuwa wanahamia Porini na kama ukichelewa inabidi upande darini kwenye nyumba hadi waondoke!

    ReplyDelete
  6. Jambo linguine kuwa la kujifunza kwa Askari wa Mkoloni hakukuwa na Rushwa!

    Ile tu Askari amekosea kwenye Gwaride anawajibishwa papo kwa hapo kwa kupigiswa push-up, sasa je iwe kwenye kosa nyeti kama la Rushwa mnafikiri ingekuwaje?

    ReplyDelete
  7. Ohhh Mshike mshike wa Majeshi ya Kikoloni walikuwa wakitekeleza Mafunzo na kuitikia amri kwa ari.

    Siyo Mafunzo wa zama hizi Polisi wanapewa mafunzo siku ya Gwaride la kuhitumu nakuwa wakakamavu wawanavunja Matofali kwa mikono na kwa kichwa halafu wakiingia mitaani ukakamavu wa kuvunja matofali kwa mikono unayeyuka wanaanza kupokea rushwa na mikono inakuwa laiiini kama mrenda!

    ReplyDelete
  8. WALIPENI POSHO NA MSHAHARA WA KUTOSHA,UTAONA JINSI ASKARI WETU WALIVYO MAKINI NA WAZURI SANA.MNATEGEMEA MAZURI TU WAKATI MNAWALIPA KIDUCHU NA WANALALA KTK KOTA ZA MABATI....HOOOVYO!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...