Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akimtangaza Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho hilo,ambaye ni Selestin Mwesigwa (aliewahi kuwa katibu mkuu wa Yanga) (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Kisheria ya TFF,Wakili Evodius Mtawala (kulia) wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.Kushoto ni Afisa Habari wa TFF,Boniface Wambura.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Kisheria,Wakili Evodius Mtawala nakala ya ilani yake ya uchaguzi wakati akimtambulisha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.kushoto ni Katibu Mkuu wa Mpya wa TFF,Selestin Mwesigwa.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu wa TFF, Selestin Mwesigwa nakala ya ilani yake ya uchaguzi wakati akimtambulisha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
NANI MTANI JEMBE SASA??Hongereni wote mlioteuliwa na hasa wewe rafiki yangu Mwesigwa mzee wa Hall 6.Umekula shavu mkuu,chapa kazi achana na 'ushabiki' wa SIMBA na YANGA
ReplyDeleteDavid V
Inakuwaje katiba ya TFF inaruhusu mtu aliyekuwa na maslahi kwenye club inayoshiriki ligi kuu kuwa katibu mkuu? Je hii sio mgongano wa maslahi?
ReplyDelete