Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
MKE NA MUME KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA KEMIKALI YA ETHANOL
Moshi. Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni mume na mke, wanakabiliwa na mashtaka matatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, yakiwemo ya kumiliki lita 704.5 za kemikali inayodhaniwa kuwa ni Ethanol kinyume cha sheria. Katika kesi hiyo, Thadey George Lekule (52), mkazi wa Longuo B, Moshi mkoani Kilimanjaro, amefikishwa mahakamani leo Jumatano Mei 7, 2025 na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Rehema Olambo. Hata hivyo, mshtakiwa wa pili, Evalyin Thadey Lekule (47), hakufika mahakamani, ambapo ilielezwa kuwa ni mgonjwa na yupo Rombo kwa matibabu. Kutokana na kutofika kwa Evalyin, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Bora Mfinanga, uliomba kesi kuahirishwa kesi hiyo hadi atakapopatikana. Hata hivyo, Hakimu Olambo alikataa ombi hilo, akieleza kuwa haitakuwa sahihi kuahirisha shauri lililowasilishwa kwa mara ya kwanza mbele yake. Hakimu alielekeza kusomwa kwa maelezo ya awali kwa mshtakiwa aliyepo, Thadey, huku akimtaka kuhakikisha kuwa mkewe anafika mahakamani kesi hiyo itakapotajwa tena. Ameonya kuwa endapo hilo halitatekelezwa, hatua kali zitachukuliwa. Wakili Mfinanga akisoma maelezo ya awali amedai mahakamani hapo kuwa Januari 31, 2025, katika eneo la Shanty Town, Moshi, mshtakiwa Thadey alikutwa na kemikali inayodhaniwa kuwa ni Ethanol kinyume cha Sheria ya Kudhibiti Dawa za Kulevya. Shtaka la pili linamhusisha na kumiliki kemikali hiyo bila usajili rasmi, na la tatu linahusu kumiliki kemikali hiyo katika eneo ambalo halijasajiliwa kisheria. Wakili wa Serikali alibainisha kuwa makosa hayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria, hasa ikiwa kiasi kilichokutwa kinazidi lita 30. Hivyo, mshtakiwa ataendelea kushikiliwa hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Mei 20, 2025. Imeandaliwa na Ombeni Daniel

Mwananchi Digital

1.16M subscribers
Chat Replay is disabled for this Premiere.