Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
KIAMA KAMPUNI 95 ZA UCHIMBAJI MADINI, MAVUNDE AWAPA SIKU SABA
0Likes
181Views
May 62025
Huenda kampuni 95 zikapoteza leseni zake za uchimbaji wa madini, ikiwa zitashindwa kujieleza kwa nini wasifutiwe leseni zao ndani ya siku 30. Kampuni hizo zilipewa hati ya makosa ambayo inazitaka kujibu hoja za kutofutiwa leseni Aprili 14 mwaka huu ambazo zinatarajiwa kufikia tamati Mei 13, 2025. Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Madini, Antony Mavunde wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya hatua wanazokwenda kuchukua dhidi ya wawekezaji wa sekta hiyo ambao wamekiuka mikataba waliyoingia. Mavunde amesema Serikali imetoa leseni kwa wawekezaji wa kati na wakubwa ili kufanya uchimbaji nchini, lakini baadhi ya wamesaini mkataba na hawajaanza kufanya kazi kinyume na sheria. “Zipo kampuni kubwa zimesaini mikataba hii lakini hawajaanza utekelezaji wa miradi yao hadi leo. Serikali imetoa hati za makosa kwa wamiliki wa leseni 95 na kuwapa siku 30 ili kama wana hoja ya kujibu kupitia hati hii ya kutoanza shughuli za uchimbaji madini nchini walete majibu yao,” amesema.

Mwananchi Digital

1.17M subscribers