Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limesema kuwa shambulio la Katibu Mkuu wake, Padri Charles Kitima, si la kawaida kwani linagusa utu wa mtu, heshima ya taasisi na sifa ya Taifa.
Padri Kitima alivamiwa na kushambuliwa Aprili 30, 2025 katika makao makuu ya baraza hilo, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa leo, Jumapili Mei 4, 2025 na Makamu wa Rais wa TEC, Askofu Eusebius Nzigilwa, katika hafla ya kumsimika Askofu Stephano Musomba kuwa kiongozi wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais Dk Philip Mpango.
“Tukio hilo si la kawaida. Linagusa utu wa mtu, heshima ya taasisi na sifa ya Taifa letu. Huu haukuwa wizi wa mali, bali ni jaribio la kupoka uhai, uhuru na haki ya kuishi kwa dhamiri na imani,” amesema Askofu Nzigilwa huku akitoa wito kwa vyombo vya dola kushughulikia tukio hilo kwa uzito.
Video na Khatibu Mgeja. …...more
...more
Show less