Mchungaji Dk Eliona Kimaro wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amesema kuwa katika zama hizi za mmomonyoko wa maadili, Afrika imebaki kuwa tumaini la dunia na Tanzania kuwa msingi wa matumaini hayo kwa uthabiti wake katika misingi ya maadili.
Akizungumza leo, Jumanne Aprili 22, 2025 jijini Dar es Salaam katika kikao kazi cha maofisa utamaduni na maofisa maendeleo ya michezo Tanzania kinachofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan. Dk Kimaro amewasilisha mada kuhusu mmong'onyoko wa maadili, akisisitiza umuhimu wa jamii kuzingatia misingi ya maumbile na utambulisho wa binadamu.
"Tumaini la dunia kwa sasa ni Afrika. Kujua kwamba mtu anayeweza kusema kwa uhakika kuwa 'mimi ni mwanaume' au 'mimi ni mwanamke' lipo Afrika, na tumaini la Afrika lipo Tanzania," amesema Dk Kimaro. …...more
...more
Show less