Wananchi wa Mabogini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamefunga barabara kwa zaidi ya saa tatu leo Aprili 17, 2025, wakilalamikia mkandarasi wa barabara kuelekeza mitaro ya maji kwenye makazi yao.
Wakazi hao wamefunga barabara ya Spenconi-Fonga gate-Mabogini-Kahe wakitaka serikali iingilie kati na kuhakikisha maji yanaelekezwa kwenye Mto Njoro ili kuondoa athari za mafuriko wanazokumbana nazo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Fatuma Omary, mmoja wa wakazi, amesema mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo imesababisha maji kuingia ndani ya nyumba zao na kuharibu mali, hali iliyowalazimu kukesha.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava amewasili eneo hilo pamoja na wataalamu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) na Bonde la Pangani na kuagiza ndani ya siku mbili mfereji unaoelekeza maji mtoni ukamilike.
Meneja wa Tarura Wilaya ya Moshi, Cuthbert Kwayu, amekanusha madai kuwa mitaro imeelekezwa kwa wananchi na kusema athari zimechangiwa zaidi na mto kujaa.
Video na Ombeni Daniel. âŚ...more
...more
Show less