Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
Wazazi wawachongea wanaowapa wanafunzi dawa za kuzuia mimba
Baadhi ya wazazi wilayani Pangani mkoani Tanga wameomba Serikali kuangalia jinsi ya kuwasaidia wanafunzi wa kike wilayani humo kutokana kuibuka tabia ya kutumia dawa za kuzuia mimba katika umri mdogo. Wakizungumza baadhi ya wazazi wa Kata ya Mkaramo wilaya ya Pangani leo Ijumaa April 11, 2025 kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na mawakili wanaosikiliza kero na changamoto za wananchi kupitia kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia wamefichua kuwa wapo wanawake wanafanya hivyo kwa watoto wao wa kike ambao bado ni wanafunzi. Mmoja wa wanawake wa Kijiji cha Mkalamo Anjelina Yohana amekiri wapo baadhi ya wazazi wanahusika na vitendo hivyo kwenye eneo hilo na mbinu hiyo inafanyika kwa siri ili kuwakinga kupata ujauzito. Mkazi wa Pangani Anastadhia Maganga amesema sababu ya baadhi wa wanawake kufanya hayo ni kutokana na kuchukua mikopo na kushindwa kurudisha hivyo wanawatumia watoto kama chanzo cha kipato kwa kuingiza chochote. Akiwa kwenye mkutano huo, Mratibu wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia Wilaya ya Pangani Judith Kapaga amekiri changamoto hiyo kuwepo kwenye maeneo mengine aliyopita, kwa wanafunzi wa kike kukutwa na vidonge vya P2 kwenye mabegi yao. "Watoto kwenye mabegi tumewakuta na P2 na dawa nyingine za kuzuia mimba na wale wa kiume wamekutwa na mipira ya kiume mifuko ya pembeni kwenye mabegi," amesema Judith. Imeandikwa na Rajabu Athumani

Mwananchi Digital

1.16M subscribers
Chat Replay is disabled for this Premiere.