Sign in to confirm you’re not a bot
This helps protect our community. Learn more
WAKRISTO WATAKIWA KUTOHUKUMU WAMUAGA BRUDA MAUKI
Makamu Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Salvinus Kwembe amewataka Wakristo kuepuka kuhukumu wengine badala yake waishi kwa kufuata mafundisho ya dini, wakitenda mema na kuishi kwa hofu ya Mungu. Askofu Kwembe ametoa wito huo wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa Bruda Mauki, aliyefariki Aprili 3, 2025 baada ya kugongwa na bajaji eneo la Area Six, Morogoro. Bruda Fidelis alizaliwa Julai 16, 1957 Materuni, Moshi Vijijini. Alijiunga na Utawa wa Mt. Fransisko na aliweka ahadi ya maisha ya kitawa Julai 9, 2000. “Fidelis alikuwa na uimara wa kiimani ambao tutaendelea kuuenzi,” amesema Pius Mauki, mdogo wake. Katekista Frolin Chembele amesema: “Unyenyekevu wake na moyo wa kujitolea kufundisha elimu ya dini ni mambo tutakayomkumbuka nayo." Video: Jackson John

Mwananchi Digital

1.16M subscribers
Chat Replay is disabled for this Premiere.