Baada ya uzinduzi wa barabara ya Migori-Iringa ambayo ni sehemu ya Barabara ya Dodoma hadi Iringa, Mhe Rais alizungumzia nia yake ya kuhakikisha Utalii unanyanyuka Southern Circuit ambapo Mkoa wa Iringa ndio kitovu.

Kati ya mambo ambayo Serikali imedhamiria kuyafanya ni pamoja na kuufanya uwanja wa ndege wa Nduli kuwa mkubwa na wa kisasa, na kujenga barabara ya Iringa hadi geti la Ruaha National Park.

Hatua hizi ni wazi kuwa zitaifungua Iringa kifursa mbalimbali. Ni muhimu kuanza kujiweka sawa kuanzia mafunzo katika masuala ya Utalii.Ni wajibu wetu kuwa-encourage vijana wetu kujihusisha na masuala ya Utalii ikiwa ni pamoja na kujifunza lugha za nje kama Kispaniola, kifaransa, kijerumani nk

Ukienda Zanzibar kwa mfano, kuna vijana wengi sana wamejikita katika shughuli za utalii kama kuongoza watalii nk. Vijana hao wamefanikiwa kwa sababu waliona hiyo fursa na kuichangamkia japo kwa kupata basic courses za masuala ya Utalii.

Kwa mujibu wa taarifa za Serikali, mpaka kufikia 2017, sekta ya utalii ndio ilikuwa inaongoza kwa kuliingizia Taifa fedha za kigeni, kiasi cha zaidi ya 17%. Kwa hiyo kuna fursa katika Utalii. Iringa na maeneo/mikoa ya jirani tujiandae katika kuchangamkia fursa hii inayokuja mbele yetu.

Cosato Chumi
Mafinga Mjini
30 April, 2018
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mafinga Mhe.Cosato Chumi mapema jana mara baada ya kuwasili mkoani Iringa 

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...