Aliyekuwa kocha Simba Patrick Liewig (pichani) amerejea nchini na kuitaka klabu hiyo imlipe malimbikizo ya mshahara wake kisha iachane naye kwa amani.

Simba iliachana na  Liewig baada ya kutoridhishwa na matokeo ya mechi za msimu uliopita na kuishia kukamata nafasi  tatu.

Akizungumza na Ripota wetu mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam jana alfajiri,Liewig alisema,hawezi kulazimisha Simba imwongezee mkataba  isipokuwa anachohitaji ni malipo ya malimbikizo ya mishahara yake.

"Nimekuja hapa kwaajili ya kutaka kujua kinachoendelea, sababu nimesikia tu  juu juu kuwa sitakiwi kwenye timu na sijaambiwa rasmi.

"Pamoja na hayo mimi sina tatizo,kama wameamua hivyo kuachana na mimi sawa isipokuwa wanilipe fedha zangu ninazodai kwani ni haki yangu na ndio maana nimekuja Tanzania"alisema Liewig

Aliongeza" Mkataba wangu umeisha Juni lakini kuna fedha zangu bado nawadai hivyo siwezi kuziacha hivi hivi, lazima wanilipe ndipo tumalizane kwa amani".

Kocha huyo aliichukua Simba mikononi mwa kocha aliyetimuliwa Milovan Cirkovic na alianza kuinoa timu hiyo kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo alisifika kwa ukali wake kwa wachezaji na hivyo kuamua kufanya uamuzi mgumu wa kuwasimamisha baadhi ya wachezaji nyota wa timu hiyo kwa madai ya utovu wa nidhamu na kuwatumia vijana katika michezo  10.

Hata hivyo habari za ndani zinadai kuwa kocha huyo anaidai klabu hiyo malimbikizi ya mshahara wa miezi mitatu unaofikia kiasi cha dola 36,000.
Kaimu Makamu mwenyekiti wa Simba Joseph Itangare alisema hawana taarifa ya ujio wa kocha huyo lakini wanasubiri kama atawasiliana nao basi watamsikiliza.

"Sisi hatujui kama amefika hapa nchini lakini tunangoja kama atawasiliana na sisi tutafanya mazungumzo naye" alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2013

    mishahara hawalipi wanategemea kocha atafundishaje na njaa na mawazo pia kama sio kujitakia

    wao mabosi wanakula na kuiba

    wamlipe baba wa watu aondoke, wana tia aibu Tanzania na kufukuza wengine wakitaka kuja nchini kwa chochote.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2013

    Mlipeni pesa yake aondoke zake na msijibalaguze eti hamjui kama yupo...mnajua sana acheni dhuluma za wazi, mpeni chake aanze wezi wakubwa nyie

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2013

    Makubwa haya jamani!!!! Mtu anadhulumiwa haki yake hivi hiviiiii bila haya!! Inamaana mpaka leo hii mnataka watu wafanye kazi bila kulipwa? Mnatia aibu kutokumlipa babu wawatu! Mpeni chake asepe wacheni kujifanya machizi. Sasa kapoteza nauli yake kuja kudai hela hapo bado chakula, malazi na usafiri!!! Hakika mnatia aibu sana.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2013

    Mlipeni upesi. Kujua au kutojua kama amekuja haiwaondlei liability ya kumplipa pesa zake za mshahara amazowadai. Yaani mnamfanyisha kazi kocha miezi mitatu bila kumpilipa na bado mnategemea matokeo mazuri kutoka kwakwe? Lo! Mnatia aibu sana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2013

    SINA CHA KUONGEZA YOTE YAMESHA SEMWA!!

    MAMBO MENGINE AIBU.\

    MDAU SIMBA - CM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...