Mwanadada Rosemary Mizizia anakualika katika Libeneke lake la Mama na Nyumba upate kujua haya na yale kuhusu nyumba na unyumba na pia kuchangia katika mada zilizomo. Kumtembelea BOFYA HAPA

Globu ya Jamii inampongeza Dada Rosemary kwa kuwa na blog iliyo tofauti na nyingi, hasa ikizingatiwa kuwapo kwa ile dhana potofu kwamba blogs ni kuhusu habari tu. Kuna mada kibao bado hazijaguswa na  zinahitaji wana libeneke kuzishughulikia. 

Mfano, ukiwa wewe ni seremala, mvuvi ama mshona viatu, fungua blog inayohusu hayo unayoyajua na kamwe hutokosa wasomaji. Nasema haya kwa kuona wengi wanapenda Libeneke tatizo wanadhani blog ni mambo ya habari tu, wakati sio kweli. Blog ni ya kila jambo ama kitu.

Mbaya zaidi wengi hawana taaluma, vifaa na hata fursa ya kupata habari lakini wanapenda kuleta habari. Wako huru, sawa, kufanya watajkalo lakini dhambi kubwa ya kwanza ya kuendesha blog ni kuwa bingwa wa copy & paste habari na picha za wengine, tena bila idhini. 

Ushauri kwa anayetaka kuendesha blog ni kuwa na mada yake, jua wasomaji wako na zaidi ya yote, usikose kuweka kitu kipya kila siku ama hata kila saa, ukiweza, ili usiboe wasomaji. Inapendeza kuwa na blogs nyingi iwezekanavyo, mradi isiwe 'sare sare maua' kama ilivyo sasa, ambapo utakuta habari ile ile katika kila blog unayosoma... 

Usiogope wala usikate tamaa kwa kudhani usipoandika mambo ya habari utakosa wasomaji.Ondokana na dhambi hiyo kuu nawe utaona matunda yake. Kwa msaada wa promotion  na ushauri, wa bure, usisite kuwasiliana nasi kupitia  issamichuzi@gmail.com
-Ankal

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...