Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza kuwa Skauti Mkuu nchini.
Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi wa Mheshimiwa Mahiza umeanza tangu tarehe 19 Aprili, 2013.
Mheshimiwa Mahiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu ambaye amemaliza muda wake.
Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Kila la kheri uihudumie nchi ili vizazi vijavyo waikute sehemu nzuri ya kuanzia
ReplyDeleteduh jamani kila nafasi anapewa kiongozi aliyepo madarakani,kwa nn wasiwape vijana nafasi hizi ambao bado ni wakakamavu.
ReplyDeleteHongera sana Mama Mahiza
ReplyDelete